Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Siwezi kuondoka Jiji kinyume na Kanuni – Meya Isaya
Habari za SiasaTangulizi

Siwezi kuondoka Jiji kinyume na Kanuni – Meya Isaya

Spread the love

ISAYA Mwita Charles, ameendelea kusisitiza kuwa yeye bado ni meya halali wa Jiji la Dar es Salaam na kuingeza, “nitaendelea kuhudhuria na kuongoza vikao vyote vitakavyoitishwa ambavyo ni mwenyekiti.” Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam  …(endelea).

Amesema, “nitaendelea kuhudhuria vikao hivyo kwa kuwa mimi bado ni mjumbe halali. Nitahudhuria kwa kuwa ni haki yangu ya kikatiba na kikanuni, inayotokana na kuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam.”

Isaya alitangazwa kung’olewa katika jaribio haramu la tarehe 9 Januari mwaka huu. Tokea wakati huo, kumeibuka mvutano kati ya baadhi ya wajumbe wa upinzani na wale wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Meya huyo ametoa kauli hiyo leo tarehe 18 Januari 2020, katika mazungumzo yake na MwanaHALISI ONLINE, siku moja baada ya mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Fedha ya Jiji hilo, Saed Kubenea, kusisitiza kuwa Isaya ndiye meya halali wa Jijini Dar es Salaam.

Kubenea ambaye pia ni mbunge wa Ubungo, alimtuhumu mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Spora Liana, kuubeba mgogoro huu kwa maslahi yake binafsi. 

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Chadema, Kanda ya Pwani, jana tarehe 17 Januari 2020, Kubenea alisisitiza kuwa njama zote za kumuondoa Meya zinaongozwa na mkurugenzi huyo zinalenga maslahi binafsi.

Akijibu swali la anawezaje kuendelea kutimiza majukumu yake wakati tayari amenyang’anywa gari na kufungiwa ofisi, Meya Isaya anasema, “kila kilichokuwa haki yangu, najiandaa kukidai” na kuonya kuwa ikiwa hataweza kupewa kwa hiari, atatumia njia nyingine kuzirejesha. Hakutaja njia atakazotumia.

Hata hivyo, Isaya amesema, amepanga kumwandikia barua Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Sipora Liana, kumtaka kumrejeshea haki hizo, likiwamo gari. 

Meya huyo ambaye ameingia Jiji kutokea Kata ya Vijibweni, katika halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, amedai kuwa ameamua kuchukua uamuzi huo baada ya kumuomba mkurugenzi wake amrejeshee gari hilo kwa zaidi ya mara moja.

 “Mkurugenzi nimemuomba mara zote kunipa gari langu. Hajafanya hivyo. Nafikiria kumlima barua Jumatatu wiki ijayo,” ameeleza Isaya na kuongeza, “pale Jiji hapatakalika, ikiwa hawatanirudishia haki zangu.”

Sipora alimpora Isaya gari alilokuwa akilitumia tarehe 9 Januari mwaka huu, muda mfupi baada ya jaribio la kumng’oa kugonga mwamba.

Amesema, alifanyiwa dhambi kubwa kuondolewa kwenye kiti chake kinyume cha taratibu. Amelalamikia pia kikao cha Kamati ya Fedha kufanyika chini ya ulinzi wa Polisi.

“Wananchi wa Dar es Salaam walipanga foleni kunichagua. Mkurugenzi na watu wengine wachache wenye maslahi binafsi, hawawezi kuniondoa kihuni namna hii,” amesisitiza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!