January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sitta akabidhiwa mgogoro wa CHAKUA, SUMATRA

Waziri wa Uchukuzi, Samwel Sitta

Spread the love

MGOGORO unafukuta kati ya Chama cha kutetea abiria nchini (CHAKUA) na Mamlaka ya usafirishaji wa majini na nchi kavu (SUMATRA). Mgogoro wa sasa, unahusu gharama za usafirishaji abiria baada ya bei za mafuta kushushwa. Sarafina Lidwino, anaandika.

Samwel John Sitta, waziri wa uchukuzi, ameombwa kuingilia katika mgogoro huu kwa madai kuwa Sumatra wameshindwa kulinda maslahi ya abiria.

Mwenyekiti wa CHAKUA, Bw. Hassan Mchanjama anasema, pamoja na kupungua kwa bei ya mafuta, lakini nauli ya abiria imebaki palepale.

Mamlaka ya udhibiti wa nishati na maji (EWERA), imetangaza kushuka kwa bei za mafuta kutoka Sh.  2,200 kwa lita hadi Sh. 1,768.

Mwenyekiti huyo amesema, tayari wamefanya utafiti na kugundua kuwa bei ya nauli inaweza kupungua kwa asilimia 25 bila wenye magari kuathirika.

“Tumetaka kuwapo kwa punguzo la asilimia 25 la nauli kwa abiria wa nchi kavu na majini. Tunataka nauli iwe Sh.300 badala ya 400 jijini Dar es Salaam na mikoani ipunguzwe kutoka Sh.40,000 hadi Sh. 30,000,” ameeleza.

Kushuka kwa bei za nauli kutasaidia pia kushusha kwa bei za bidhaa ikiwamo chakula; na kwamba mfumuko wa bei unachangiwa kwa kiwango kikubwa na gharama za usafirishaji.

Akijibu madai hayo, Meneja Mawasiliano wa Sumatra, David Mziray, ameliambia MwanaHALISI Online kuwa malalamiko hayo yamepokelewa na ofisi yake; na kwamba barua iliyowasilishwa haina hoja za msingi kuunga mkono.

error: Content is protected !!