Monday , 27 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sita wadakwa kwa utakatishaji fedha Bil 4.78
Habari za SiasaTangulizi

Sita wadakwa kwa utakatishaji fedha Bil 4.78

Spread the love

 

WATU sita wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kwa madai ya utakatishaji fedha kiasi cha Sh. 4.78 Bil. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Pia washtakiwa hao waliofikishwa mahakamani na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), wanatuhumiwa kuongoza genge la uhalifu wa benki na udanganyifu.

Washtakiwa watano kati yao ni wafanyakazi wa Kampuni ya Peertech ambao ni Mark Julius Mposo (mkurugenzi) 40); Baraka Madafu (uendeshaji), Lusekelo Mbwele (meneja wa fedha).

https://www.youtube.com/watch?v=6Dd-qHEluOA

Wengine ni Leena Joseph (meneja operesheni) na Bernard Mndolwa (mkurugenzi wa ndani). Mshtakiwa wa sita ni Salvina Karugaba (46), mfanyakazi wa benki ya NBC, Tawi la Mnazi Mmoja.

Watuhumiwa hao wamefikisha mahakamani hapo na Takukuru Makao Makuu kwa kushirikiana na Ofisi ya Mashtaka Tanzania, leo tarehe 25 Februari 2021.

Watu hao wamesomewa mashtaka 11 katika Kesi ya Uchumi Na. 13/2021, na Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Kassian Matembele.

Miongoni mwa mashtaka waliyosomewa watuhumiwa hao ni kuongoza genge la uhalifu kati ya tarehe 4 Disemba 2018 na 31 Disemba 2020, kwenye maeneo tofauti jijini Dar es Salaam kisha kujipatia Sh. 4,78 bilioni kutoka  Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), kwa njia ya udanganyifu.

Shitaka lingine ni kughushi nyaraka za makubaliano ya dhamana zilizotolewa tarehe 6 Februari 2019, zilizokuwa na lengo la kuwatambulisha watu 60 kama wanufaika wa makubaliano hayo.

Kwamba, ni waajiriwa wa Kampuni ya Peertech, huku wakijua ni uongo. Wanadiwa kutenda kosa hilo maeneo ya Masaki, jijini humo.

Watuhumiwa hao sita wanadaiwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kati ya tarehe 4 Disemba 2018 na 31 Disemba 2020 jijini Dar es Salaam.

Na kuwa, kupitia njia za udanganyifu, walijipatia Sh. 4,78 bilioni kutoka NBC, baada ya kuwasilisha nyaraka za uongo  zinazoonesha kwamba watu 78 ni waajiriwa wa kudumu wa kampuni hiyo.

Hivyo, kampuni hiyo imewadhamini kupata mkopo kutoka katika benki hiyo, huku wakijua ni uongo.

Shitaka lingine ni utakatishaji fedha kiasi cha Sh. 4,78 bilioni ambapo inadaiwa, kati ya tarehe 4 Disemba 2018 na 31 Disemba 2020 katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam, kwa pamoja walitakatisha Sh. 4,78 kinyume cha sheria.

Baada ya Wakili Kadushi kuwasomea mashtaka watuhumiwa hao, alisema upande wa Jamhuri unaendelea kukamilisha upelelezi dhidi ya watuhumiwa hao.

Hakimu Matembele ameahirisha kesi hiyo hadi tarehe 12 Machi 2021, itakapotakuja kutajwa tena.

Aidha, Hakimu Matembele amesema, watuhumiwa watarudishwa rumande kutokana na dhamana yao kuzuiliwa kwa sababu ya kuwa na mashtaka ya utakatishaji fedha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kasekenya aipa Tanroads wiki kukarabati barabara Morogoro

Spread the loveNaibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ametoa wiki moja...

Habari za SiasaTangulizi

‘Aliyemtonya’ Lissu kuhusu rushwa arejea madarakani

Spread the loveMwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Iringa, William Mungai...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Tutaendelea kupigania malengo ya afrika

Spread the loveRais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema dhamira ya Tanzania...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NHC yadai bil. 2.1 taasisi za Serikali, Waziri atoa maagizo

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii...

error: Content is protected !!