April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Sisikii tena ‘vyuma vimekaza’- Dk. Mpango

Dk. Philip Mpango

Spread the love

DAKTARI Phillip Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango ameeleza kwamba, sasa hivi hasikii tena malalamiko ya ‘vyuma kukaza’ kutokana na benki za biashara kushusha riba. Anaripoti Martin Kamote … (endelea).

Dk. Mpango ametoa kauli hiyo leo tarehe 19 Agosti 2019 wakati akizundua kanuni za utendaji za huduma za benki, zilizoandaliwa na Chama cha Wakuu wa Benki nchini Tanzania (TBA).

Akifafanua kuhusu kauli hiyo, Dk. Mpango amesema kitendo cha benki hizo pamoja na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kushusha riba kimeongeza ukwasi, hali iliyoongeza mzunguko wa fedha.

Dk. Mpango amezipongeza benki hizo kwa kushusha riba, na kuzitaka taasisi nyingine za fedha kushusha viwnago vya vya riba ili kuwapunguzia mzigo wananchi.

error: Content is protected !!