May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Siri ya uwezo wa Hamza kutumia AK47 yafichuka

Hamza Mohamed, aliyefyatulia risasi Polisi na kuwaua

Spread the love

 

SIRI ya Hamza Hassan Mohamed kumudu kutumia silaha na kuwaua askari watatu wa jeshi la polisi na mlinzi mmoja wa kampuni ya ulinzi ya SGA jijini Dar es Salaam kisha mwenyewe kuuawa, imebainika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Muuaji huyo ambaye uchunguzi wa tukio lake linaendelea kuchunguzwa na Jeshi la Polisi aliibua maswali mengi likiwamo wapi alikopata uwezo wa kutumia silaha za moto kwa namna alivyoonesha.

Lakini pia bado kuna maswali ambayo yanaendelea kuzunguka katika vichwa vya Watanzania ni kwanini aliamua kushambulia askari polisi pekee huku wananchi wengi wakiwepo.

Siku ya tukio hilo, Jumatano ya wiki iliyopita, Hamza alitumia bastola yake binafsi kuwafyatulia risasi askari polisi hao na kusababisha vifo vyao papo hapo.

Baada ya kuwaua, Hamza alipora silaha mbili bunduki aina ya AK 47 ambapo moja aliitundika shingoni, bastola kuunoni na bunduki nyingine aliishika mbele yake.

Undani wa habari hii soma Gazeti la Raia Mwema toleo la leo Jumatatu tarehe 30 Agosti 2021.

error: Content is protected !!