July 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Siri wana-UDOM kutimuliwa hadharani

Spread the love

SABABU za wanafunzi 7,800 wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kutimuliwa sasa zipo hadharani,ananadika Aisha Amran.

Ni kutokana na kuwepo kwa mgogoro kati ya chuo hicho na wafanyakazi wake ambao umekwenda moja kwa moja kuathiri wanafunzi hao.

Chama cha Taasisi za Elimu ya Juu, Tawi la UDOM (THTU) kimeeleza kuwa, mgongano uliopo kati ya viongozi wa chuo hicho na wafanyakazi wake.

Ni kutokana na walimu wanaofundisha wanachuo hao kutolipwa fedha zao na chuo jambo lililosababisha kuchelewa kuendelea na masomo na hata kuibua mgogoro huu.

Hivi karibuni UDOM kilitoa taarifa ya kusimamisha wanafunzi hao wa kozi maalumu ya ualimu wa Sayansi, Hisabati na Teknolojia kwa ngazi ya Stashahada na kisha kutaka waondoke chuoni hapo mara moja.

Tangazo hilo lilieleza kuwa, kutokana na matatizo yaliyopo katika ufundishaji wa stashahada hiyo, Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi imeamua wanafunzi hao kurejeshwa majumbani na kwamba wataelezwa mustakabali wao.

Kozi ya Stashahada ya Ualimu wa Sayansi, ilianzishwa maalumu kwa agizo la Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete kwa lengo la kuziba pengo la walimu wa sayansi na ilikuwa inatolewa UDOM pekee.

Taarifa ya THTU iliyosainiwa na Nashon Chache, mwenyekiti wake inaeleza kuwa, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma (DVC-ARC) ndio chanzo kutokana na kushindwa kutoa ushirikiano ili kuhakikisha kazi zinakwenda kama zilivyotarajiwa.

Pia mwingine anayetajwa kuwa sehemu ya tatizo hilo ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala (DVC-PFA).

Taarifa hiyo inaeleza kuwa, mgogoro huo unaweza kuwiana na ule uliotokea mwaka 20014/15 ambao ulisababishwa kuundwa kwa Kamati ya Uratibu (SC) na kwamba chama hicho kinaamini kuwa, kama ofisi ya DCV-PFA ingekuwa makini, mgogoro huo usingekuwepo.

“Badala ya kufanya kazi hii kwa ari, weledi na uaminifu kama ilivyostahili, viongozi hawa wawili wameamua kuwa waongo, wasiojali maslahi ya wanafunzi na umma na taasisi wanayoiongoza katika ujumla wake,” imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa zinaeleza kuwa, mgogoro huo ulianza wakati walimu walipotakiwa kulipwa kwa kufanya kazi ya ziada ya kuwafundishwa wanafunzi hao.

Na kwamba, kutokuwa tayari kwa viongozi hao kukaa meza moja na walimu waliokuwa wakifundisha wanafunzi hao, ndiko kulikozidisha tatizo zaidi.

“…badala yake wanamlazimisha mkuu wa chuo kutatua mgogoro bila kumpa nyenzo, bili maana yake ni kufanya mambo bora liende,” imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, kutokana na makubaliano ya mapendekezo ya kamati maalim ya uratibu, walimu hao wa ziada walitakiwa kulipwa Sh. 1,000,000 lakini haikutekelezwa.

Hivyo, mvutano wa malipo hayo ndio uliosababisha wanafunzi kuchelewa kuanza masomo yao ya muhula wa pili ambapo Makamu Mkuu wa chuo alipobaini hivyo, aliamuru malipo yafanyike ili wanafunzi waendelee na masomo.

Hata hivyo, baada ya agizo hilo, ofisi husika haikutekeleza agizo hilo jambo lililoibua matatizo mengine na hata hatua mgogoro huoo kufikia hapa.

error: Content is protected !!