March 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Sinema ya Lissu na Polisi yaendelea Dar

Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, akiwa chini ya ulinzi wa polisi

Spread the love

JESHI la polisi limeendelea kumshikilia Mwanasheria mkuu wa Chama cha Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu aliyekamatwa juzi jijini Dar es Salaam na kushikiliwa katika kituo kikuu, anaandika Hellen Sisya.

Mwanasheria huyo leo alitarajiwa kupelekwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kusomewa mashtaka yake, lakini mpaka sasa hajapelekwa huko.

Tumaini Makene, Ofisa habari wa chama hicho, amesema kwamba chama hicho kinatarajia kwamba mwanasheria huyo atapata dhamana ya polisi na kwamba hilo lisipofanyika watachukua hatua za kisheria kuhusiana na hilo.

Mpaka sasa haijulikani hatma ya Lissu japokuwa Chadema bado wanaendelea kutoa taarifa za matumaini kwamba huenda leo mwanasiasa huyo anaweza kupata dhamana ama polisi au mahakamani.

error: Content is protected !!