May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simulizi ya mwanasiasa mkongwe wa upinzani, Anthony Komu

Spread the love

 

ANTHONY Calist Komu, mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania amesema, ndoto zake zilikuwa awe padre, lakini akajikuta anakuwa mwanasiasa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Komu ni miongoni mwa wanasiasa, walioendesha vuguguvu la kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini Tanzania, akiwa chama cha NCCR-Mageuzi.

MwanaHALISI TV na MwanaHALISI Online, limefanya mahojiano maalum na Komu, aliyezaliwa tarehe 17 Januari 1964, Moshi mkoani Kilimanjaro, akiwa ni baba wa watoto watatu na mke mmoja.

Katika mahojiano na Komu, amezungumzia sababu za kuwaita watoto wake majina ya uchaguzi, ujenzi na matawi na nini kilikwamisha ndoto zake za kuwa padre.

Pia, Komu anaeleza jinsi alivyoongoza mapinduzi ya serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, jinsi alivyoshindwa kutetea nafasi ya ubunge wa Moshi Vijijini katika uchaguzi mkuu uliopita wa mwaka 2020.

Komu alikuwa miongoni mwa waanzilishi wa chama cha NCCR-Mageuzi miaka ya 1990 hadi mwaka 2002 alipong’atuka na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Amekaa Chadema kuanzia mwaka 2003 hadi 2020 alipoamua kurejea tena NCCR-Mageuzi na sasa amechaguliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho.

Mengi zaidi kumhusu Komu, fuatilia mahojiano yake.

error: Content is protected !!