August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simu ‘feki’ zakaribia ukingoni

Spread the love

WATANZANIA wametakiwa kuhakikisha hawaendelei kununua na kutumia simu feki badala yake wawe makini katika ununuzi wa simu hizo kwani simu hizo (feki) zitazimwa Juni 16 mwaka huu, anaandika Dany Tibason.

Taadhiari hiyo ilitolewa na leo na Yahaya Simba, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu udhibiti wa simu feki.

Mbali na kuzima simu hizo amesema, siyo kweli kwamba simu ndogo za tochi zote ni feki.

Mbali na hilo amesema, kwa sasa wanaendelea na utoaji wa elimu kwa wananchi juu ya utumiaji wa simu za kiganjani na kueleza kwamba, kutokana na elimu hiyo simu feki zimepungua kutoka asilimia 30 na kufikia asilimia 18 sasa.

Hadija Ngasongwa Sijaona, Mwanasheria wa Tume ya Ushindani (FCC) amesema, kwa sasa wanaendelea kufanya ukaguzi wa kushutukiza katika maduka mbalimbali ili kubaini maduka ambayo yanauza simu feki.

Amesema simu ambazo zinagunduliwa kuwa feki zimekuwa zikikusanywa na kuteketezwa kama ilivyo kwa bidhaa nyingine feki.

error: Content is protected !!