
Mwanariadha Alphonce Simbu amekuwa Mtanzania wa kwanza kutwaa medali kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola msimu huu inayoendelea Uingereza. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Simbu amemaliza wa pili katika mbio ya marathoni kwa wanaume iliyomalizika jana tarehe 30 Julai, 2022 mjini Birmingham.
Mwanariadha huyo alikimbia kwa saa 2:12:29 na kufanikiwa kutwaa medali ya fedha akiwa nyuma ya Mganda, Victor Kiplangat aliyetwaa medali ya dhahabu akitumia saa 2:10:55.
Mkenya, Michael Githae aliyekimbia kwa saa 2: 13:16 alihitimisha tatu bora huku Mtanzania mwingine, Hamis Athuman akimaliza kwenye nafasi ya nane.
Simbu amejihakikishia bonusi ya dola 7000 ambayo ni ahadi ya Serikali kwa kila mchezaji atakayeshinda medali ya fedha kwenye michezo hiyo, huku shaba ikiwa dola 5000 na dhahabu dola 10,000.
More Stories
Ligi Kuu kuanza kutimua vumbi leo
Yanga yairarua Simba, Mayele atetema
Sherehe zimekwisha sasa tukutane Agosti 13