Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Simbachawene: Jeshi la Zimamoto semeni matatizo yenu
Habari Mchanganyiko

Simbachawene: Jeshi la Zimamoto semeni matatizo yenu

Spread the love

 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani wa Tanzania, George Simbachawene, amelitaka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, kueleza changamoto zinazokwamisha utekelezaji majukumu yake mapema, badala ya kusubiri majanga yatokee. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Simbachawene ametoa agizo hilo leo Jumatatu, tarehe 12 Julai 2021, baada ya jeshi hilo kueleza changamoto zilizokwamisha lisizime kwa wakati, moto uliowaka katika Soko Kuu la Kariakoo, jijini Dar es Salaam.

Soko Kuu la Kariakoo lilianza kuungua usiku wa Jumamosi, tarehe 10 Julai 2021 na kuathiri sehemu ya juu ya soko hilo. Hadi sasa jeshi hilo limefanikiwa kuzima asilimia kubwa ya moto huo.

Simbachawene amemuagiza Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, John Masunga, aziweke wazi changamoto zinazolikabili jeshi hilo, ili zifanyiwe kazi.

“Hili liwe fundisho, Kamishna Jenerali simamia sheria na mtoke nje mseme, kupitia fundisho hili mlilopata mchukue hatua. Mtoke hadharani mseme changamoto gani zipo,” amesema Simbachawene

Awali, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Temeke, Bakari Mrisho, alitaja changamoto zilizokwamisha jeshi hilo kuchelewa kuuzima moto huo.

Mrisho amesema, changamoto kubwa ilikuwa na mabomba ya maji ya kuzimia moto (Fire Hydrants), kushindwa kufanya kazi kutokana na kuwa na kasi ndogo ya utoaji maji.

“Hapa maeneo ya Kariakoo kuna baadhi ya Hydrants ni mbovu na baadhi zilizokuwa nzima zilikuwa hazina presha ya kutosha. Mwanzoni tulizima kwa bidii ikabakia kidogo moto kuisha lakini magari ya hapa yaliishiwa maji,” amesema Mrisho.

Mrisho amesema, baada ya mabomba hayo kushindwa kufanya kazi, jeshi hilo lililazimika kwenda maeneo ya Bandari ya Dar es Salaam na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, kwa ajili ya kuchukua maji.

“Kwenda kwenye hydtants za karibu tukakuta hazina maji, ikabidi twende bandarini na airport (uwanja wa ndege),” amesema Mrisho.

Muonekano wa soko la Kariakoo baada ya kuungua moto

Ametaja changamoto nyingine iliyokwamisha zoezi hilo, ni baadhi ya wananchi wasiokuwa waaminifu waliokwenda katika eneo la tukio kwa ajili ya kufanya uhalifu.

Pamoja na changamoto ya mrundikano wa bidhaa za wafanyabiashara barabarani, hali iliyochelewesha magari ya zimamoto kupita.

“Changamoto ya pili ilikuwa na rundo la wananchi wenye nia nzuri na ovu, lakini polisi waliwadhibiti. Changamoto nyingine tumeipata ni bidhaa zilizokuwepo katika njia zilikuwa zinapitia magari yetu, ilikuwa changamoto kubwa,” amesema Mrisho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Kasilda Mgeni anasisitiza umoja, ushirikiano Same 

Spread the love  MKUU mpya wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda...

Habari MchanganyikoTangulizi

Hii hapa kauli ya Sheikh mpya mkoa wa Dar

Spread the loveSAA chache baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya aliyekuwa Sheikh...

Habari MchanganyikoTangulizi

Breaking news! Mufti amng’oa Sheikh mkoa Dar

Spread the loveBARAZA la Ulamaa la Bakwata katika kikao kilichofanyika tarehe 1...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 120 za DMDP zaibadilisha Ilala, wananchi watoa ya moyoni

Spread the loveJUMLA ya Sh bilioni 120.7 zimetumiwa na Halmshauri ya Jiji...

error: Content is protected !!