May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simbachawene, IGP Sirro kuongoza mamia kuiaga miili ya Polisi

Spread the love

 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, George Simbachawene, anaongoza mamia ya waombolezaji kuaga miili ya askari Polisi watatu na mlinzi wa kampuni binafsi ya ulinzi ya SGA, waliofariki dunia katika tukio la mauaji lililotokea juzi Jumatano, tarehe 25 Agosti 2021. Anaripoti Mwanaharusi Abdallah, TUDARCo … (endelea).

Tukio hilo lilitokea katika makutano ya barabara za Kinondoni na Kenyatta jijini Dar es Salaam, karibu na Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania.

Miili hiyo inaagwa leo Ijumaa, tarehe 27 Agosti 2021, katika viwanja vya Polisi, Kurasini mkoani Dar es Salaam.

Mbali na Simbachawene, wengine watakaoshiriki shughuli hiyo ni, Insepekta Jenerali wa Polisi nchini (IGP), Simon Sirro na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla.

Miili ya Askari Polisi itakayoagwa ni ya, Miraji Khatib Tsingay, ambaye mwili wake utazikwa nyumbani kwao Karatu mkoani Arusha. Mwingine ni Emmanuel Keralya, atakayeziwa Mkuranga mkoani Pwani na Kangae Jackson, ambaye atazikwa mkoani Katavi.

Mwili Joseph Okotya Mpondo, ambaye alikuwa mlinzi kampuni ya SGA utazikwa mkoani Singida.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online kwa taarifa na habari mbalimbali.

error: Content is protected !!