June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simbachawene ashupalia Tanesco Dar

Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakiwa kwenye foleni ya kununua umeme

Spread the love

WAZIRI wa Nishati na Madini, George Simbachawene, amewaagiza wakurugenzi wa Mkoa wa Da res Salaam kuwachukulia hatua za kinidhamu wahandisi wa maeneo ya Tabata magengeni, Tazara na   Wilaya ya Temeke kutokana na kuwa na uwajibikaji mbovu katika maeneo yao. Anaripoti Sarafina Lidwino … (endelea).

Vigogo hao ambao majina yao hayakuwekwa wazi, wanadaiwa kuwa na utendaji mbovu wa kutotekeleza majukumu yao pindi wanapohitajika kufanya kazi za umma, na hivyo kuwajibu wateja majibu yasiyoridhisha pindi wanapopigiwa simu ya dharura.

Hatua hiyo imekuja baada ya Simbachawene kukutana na viongozi mbalimbali wa utoaji huduma ya umeme, wakiwemo wahandisi na mafundi, ambao walikutana katika chuo cha Tanesko jijini Dar.

Simbachawene amesema lengo la kuwaita pale ni kutaka kuongea nao macho kwa macho kuhusiana na matatizo ya umeme na kuwapa maagizo yake badala ya kuwatumia viongozi wao, ambao pia wanawadharau.

Amesema kuwa, kuna malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wakidai kuwa hawapati huduma ya umeme kwa wakati kutokana na uzembe unaofanywa kwa makusudi na baadhi ya viongozi.

“Tambueni umeme ni kitu cha hatari sana, sasa mnapopigiwa simu ya dhalula halafu hamfiki kwa wakati mnategemea nini? Na mbaya zaidi hao wananchi mnaowafanyia hivyo wanalipa fedha zao. Msitake tuchezeane namna hiyo jamani kila mtu afanye majukumu yake na kama akishindwa pia aseme.” ameonya.

Aidha, amesema idara ya ufundi ndio chanzo kikubwa cha matatizo kwa wananchi, kwani wamekuwa wakizembea kuimarisha miundombinu katika maeneo mbalimbali hususani maeneo ambayo nguzo zimeanguka.

“Sitaweza kuvumilia upumbavu huo, na leo nimeaza na hawa watatu wengine watafuata. Na kuanzia leo sitaki kuona gari ya Tanesco imeegeshwa baa na sehemu yoyote kama hakuna kazi,” amesema Simbachawene.

Wakati huo huo, amezungumzia suala la matatizo ya umeme yaliyojitokeza hivi karibuni, ambapo amesema yamerekebishwa na tatizo la upatikanaji wa luku halipo tena.

“Kulikuwa na mgogoro kidogo kati ya kampuni moja ya kusambaza umeme na Mamlaka ya Mapata Tanzania (TRA), ambao umepelekea kampuni hiyo kufungia huduma hiyo. Hivyo kwa sasa kuduma ya umeme inapatikana kwenye mitandao yote ya simu kama ilivyokuwa mwanzo,” amesema.

error: Content is protected !!