June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simbachawene amkabidhi Lwakatare DART

Spread the love

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene amemteua Mhandisi Ronald Lwakatare kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa mabasi yaendayo haraka Dar Es Salaam (DART). Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Akizungumza leo na waandishi wa habari, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais, Tamisemi, Rabecca Kwandu ambapo amesema, Uteuzi wa Lwakatare umefanyika Januari 4, Mwaka huu.

“Mhandisi Lwakatare anatakaiwa kuripoti na kuanza kazi mara moja.” amesema Kwandu.

Amesema, Simbachawene amefanya uamuzi huo kwa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 2(2) cha amri ya kuanzisha Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka na kwa mujibu wa tangazo la Serikali namba 120 la mwaka 2007.

Kwa mujibu wa msemaji huyo, kabla ya uteuzi huo, Mhandisi Lwakatare alikuwa Naibu Mtendaji Mkuu Bodi ya Mfuko wa Barabara akishughulikia ufuatiliaji na tathimini.

Uteuzi huo unafuatia kusimamishwa kazi kupisha uchunguzikwa aliyekuwa Mtendaji Mkuu Asteria Mlambo mnamo Desemba 23, mwaka jana.

error: Content is protected !!