Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Simbachawene acharuka ufanyaji kazi wa mazoea
Habari za Siasa

Simbachawene acharuka ufanyaji kazi wa mazoea

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), George Simbachawene
Spread the love

 

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene amewataka watumishi wa ofisi yake kufanya kazi zenye ufanisi za kuleta matokeo yenye tija badala za mazoea. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Sambamba na hilo Simbachawene amesema kazi kubwa ya watumishi wa ofisi hiyo ni kuhakikisha ufanisi wa kazi unaosababisha matokeo ambayo yatakuwa na ukweli unaoonekana machoni mwa watu.

Rai hiyo imetolewa leo tarehe 19 Januari, 2023 mkoani Dodoma, alipokuwa akizungumza na watumishi wa ofisi hiyo wakati akifungua mafunzo kwa idara ya ufuatiliaji na tathimini ya utendaji wa shughuli za Serikali iliyofanyika Dodoma.

Waziri amewataka watumishi hao kufanya kazi zao kwa kufanya tathimini na ufuatiliaji kwani jambo hilo ni sehemu muhimu katika kuchambua rasilimali zote na kuzifuatilia na kuona kama kuna matokeo yaliyotarajiwa.

Katika kikao hicho aliendelea kusisitiza kuwa ofisi nyingi za Serikali kwa kipindi cha miaka miwili kimianzisha kitengo cha ufuatiliaji na tathimni na kwamba ofisi hiyo imeanza utaratibu wa kuwajengea uwezo uwatumishi na wataalamu na menejimenti ya wizara kwa kujua mfumo huo wa ufuatiliaji na tathimini wa shughuli za serikali kwa kuhakikisha inapata majibu na malengo yaliyokusudiwa.

“Tunataka utendaji unaotatua matatizo ya wananchi hatutaki utendaji wa mazoea useme umetatua tatizo linalomgusa mwananchi na matokeo hayo ndiyo viongozi wetu wa juu wanayoyataka…kinachotakiwa ni kila mmoja kuonesha matokeo ya kweli kwa kila mtendaji wa serikali pamoja na taasisi zote za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” amesema Simbachawene.

Kuhusu mvua zinazoendelea amewataka wakulima kuendelea kutumia mvua zinazoendelea kutumia kilimo kinachokuwa na tija kwa kupanda mazao ambayo yanaendana na mazingira sahihi kwa mahali sahihi.

Mbali na hilo amewataka wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuhakikisha wanatoa matangazo kwa wakulima kutokana na taarifa zinazotolewa na Mamlaka ya hali ya hewa ili kuweza kuwapatia taarifa sahihi ambazo zinawafanya kulima wa mazao ambayo yatakuwa sahihi kwa muda huo.

Sambamba na hilo amewataka wakulima kuhakikisha wanatumia utandawazi kwa ajili ya kupata taarifa sahihi kwa ajili ya kupata masoko bora ya mazao yao ambayo wanatakiwa kuyapeleka kwenye masoko ya ndani na ya nje ya nchi.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo John Jingu, awali akizungumza na watumishi hao, amesema kuwa mafunzo hayo ya siku mbili yatawajengea uwezo watumishi, wafanyakazi pamoja na menejimenti watawaza kufanya kazi kwa ajili ya kuleta ufanisi kwa serikali na kuleta matokeo kwa serikali husika.

Jingu alisema kuwa mafunzo hayo ya siku mbili yanalenga kutekeleza majukumu muhimu ambayo yanatekelezwa zaidi na katibu na mratibu kwa kuhakikisha wanafanya kazi ya tathimini na ufuatiliaji kwa ueledi zaidi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo aungana na wananchi ujenzi maabara za sekondari

Spread the loveMBUNGE wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, kwa kushirikiana na...

Habari za Siasa

CCM apiga marufuku wazazi kuwatumia watoto wa kike kwenye mambo ya kimila

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

Ofisi za mabalozi wa mashina zitumike kuwale vijana kimaadili – Chongolo

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameagiza...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

error: Content is protected !!