October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simbachawene aagiza vyuo vya sheria kutoa msaada wa kisheria

Spread the love

WAZIRI wa Katiba na Sheria George Simbachawane ametoa wito kwa vyuo vinavyofundisha taaluma ya sheria nchini kutoa huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi kama inavyofanywa na Shule ya Sheria Tanzania (LST) kwa kutoa huduma hiyo. Anaripoti Faki Sosi …(endelea).

Waziri Simbachawene ameyasema hayo leo tarehe 10 Machi 2022, alipofanya ziara katika shule hiyo iliyopo Mawasiliano jijini Dar es Salaam.

“Nimefurahi nilipofika hapa nimeona kitengo cha msaada wa kisheria tena ni bure kabisa, rai yangu ningeomba vyuo vyote vinavyofundisha taaluma ya sheria watoe huduma ya msaada wa sheria” amesema Wazairi Simbachawane.

Amesema kuwa huduma ya msaada wa sheria ipo kwa mujibu wa sheria na kwamba Serikali imeanzisha kitengo ili kutoa msaada kwa Watanzania wenye uhitaji.

“Ofisini kwetu yupo Mkurugenzi anayeshughulika na huduma za msaada wa kisheria, vilevile anasajili watoa huduma hiyo,” amesemma Simbachawene.

error: Content is protected !!