May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yawasili Cairo kukamilisha ratiba na Al Ahly

Spread the love

 

KIKOSI cha wachezaji pamoja na viongozi wa klabu ya Simba umewasili salama jijini Cairo, Misri kwa ajili wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Al Ahly. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo wa kundi A, utachezwa siku ya Ijumaa tarehe 9 Aprili 2021 majira ya saa 4 usiku kwa saa za Afrika mashariki.

Simba inaenda kucheza mchezo huo wa kukamilisha ratiba mara baada ya kufuzu hatua ya robo fainali kwa ushindi wa mabao 4-1, dhidi ya As Vita kutoka Jamhuri ya Congo.

Mpaka sasa Simba ameshafuzu kwenye kundi hilo akiwa na pointi 13 huku akiwa kinara kwenye msimamo.

Mchezo huo utakuwa unakamilisha hatua ya makundi ambapo wenyeji Al Ahly anahitaji ushindi ili kujihakikishia kufuzu kwenye hatua ya robo fainali kama mshindi wa pili.

Katika michezo mitano Simba waliocheza kwenye hatua ya makundi mpaka sasa wamefanikiwa kushinda michezo minne na kwenda sare mmoja huku wakipachika kambani mabao tisa na kuruhusu bao moja.

error: Content is protected !!