May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yawasili Afrika kusini, walia kunyimwa Askari

Spread the love

 

KLABU ya Simba imewasili salama nchini Afrika Kusini kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Orlando Pirates, huku wakilalamika kuwa wenyeji hao wameshindwa kuwapatia polisi wa kuwaongoza barabarani (Escort). Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo wa wa marudiano wa robo fainali utapigwa siku ya Jumapili, Aprili 24, 2022 kwenye dimba la Orlando lililopo Soweto, jijini Johannesburg.

Simba ambao waliondoka nchini leo asubuhi, kupitia kurasa za mitandao ya kijamii walitoa taarifa hiyo ya kuwasili Afrika Kusini, na kuwashukuru wenyeji wao hao kwa mapokezi licha ya kutowapatia Askari.

“Asanteni Orlando Pirates kwa mapokezi lakini mmetunyima polisi wa kutuongoza barabarani (Escort) hivyo tumelazimika kutumia gari la Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya kusini kutuongoza”

Simba wanaingia kwenye mchezo huo siku ya Jumapili, huku wakiwa na kumbukumbu ya kupata ushindi kwenye mchezo wa kwanza kwa bao 1-0, uliopigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Kwenye mchezo huo Simba inahitaji sare ya aina yoyote, ili kuweza kufuzu kwa hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.

error: Content is protected !!