December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Simba yatolewa kimataifa kwa aibu, kuhamia Kombe la Shirikisho

Spread the love

 

SIMBA ya jijini Dar es Salaam nchini Tanzania imetolewa katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika kwa kipigo cha 3-1, katika Uwanja wake wa nyumbani, Benjamin Mkapa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Simba imepokea kipigo hicho kutoka kwa Jwaneng Galaxy ya Botswana leo Jumapili, tarehe 24 Oktoba 2021.

Katika mchezo wa awali uliochezwa wiki moja iliyopita nchini Botswana, Simba iliibuka na ushindi wa 2-0. Kwa kipigo cha 3-1 ilichopokea leo, Simba inakuwa imetoka kwa magoli ya ugenini.

Safari ya mwisho kwenye michuano hiyo ya Simba, imehitimishwa na 85.

Bada ya kutolewa, Simba inakwenda kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho kwa kucheza mchozo mmoja na iwapo itavuta hatua hiyo, itaingia makundi ya michuano hiyo.

error: Content is protected !!