May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yatinga robo fainali kombe la Shirikisho kibabe

Spread the love

USHINDI wa mabao 4-0, ulitosha kuifanya klabu ya Simba kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika mara baada ya kumaliza nafasi ya pili kwenye kundi lao. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mchezo huo wa kundi D, ulipigwa usiku wa kuamkia leo tarehe 3 April 2022, kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Alama hizo tatu ziliifanya Simba kufikisha jumla ya pointi 10, sawa na RS Berkane kwenye nafasi ya kwanza kwa kulinganishwa matokeo katika michezo yao waliokutana.

Kwenye mchezo huo Simba iliwalazimu kusubiri mpaka dakika 45 za kipindi cha pili, mara baada ya kushindwa kupachika mpira nyavuni kwenye kipindi cha kwanza cha mchezo licha ya kupata nafasi nyingi.

Bao la kwanza la Simba kwenye mchezo huo liliwekwa kambani na Sadio Kanout kwenye dakika ya 63, huku Chriss Mugalu akipachika bao la tatu na la nne kwenye dakika za 68 na 79.

Simba haikuishia hapo tu, mara baada ya kufanya mashambulizi langoni mwa Us Gendarmerie, mnamo dakika ya 84 mlinda mlango wao alijikuta kwenye wakati mgumu mara baada ya kujifunga.

Mara baada ya matokeo hayo Simba itasubiri Droo ili kujua itakutana na nani kwenye mchezo war obo fainali wa michuano hiyo ya pili kwa ukubwa kwa ngazi ya klabu barani Afrika ambayo itachezwa wiki mbili zijazo.

error: Content is protected !!