November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yatawala tuzo kombe la Mapinduzi

Spread the love

 

LICHA ya kutwaa taji la kombe la Mapinduzi, klabu ya soka ya Simba imetwaa tuzo tatu muhimu kwenye michuano hiyo ambayo imeunguruma kwa wiki mbili visiwani Zanzibar. Anaripoti Mwandishi Wetu….(endelea)

Simba ilitwaa ubingwa huo kwenye mchezo wa fainali mbele ya Azam FC, mara baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0, bao lilifungwa na Meddie Kagere.

Mara baada ya kukamilika kwa michuano hiyo, Simba ilifanikiwa kutwaa Mfungaji bora wa mashindano ambaye ni Kagere mwenye mabao matatu katika michezo minne waliocheza.

Simba haikuishia kwenye tuzo hiyo tu, bali ilifanikiwa pia kutoa mchezaji bora wa michuano hiyo ambaye ni Pape Ousmane Shakho.

Katika michuano hiyo Sakho alikuwa kwenye kiwango kizuri mara baada ya kutwaa mara mbili tuzo za mchezaji bora wa mechi na kupachika mabao mawili kwenye michuano hiyo.

Aidha kwa upande wa tuzo ya mlinda mlango bora ilikwenda kwa Aishi Manula ambaye amecheza michezo mitatu bila kuruhusu bao lolote langoni mwake.

Taji hilo linakuwa na nne kwa Simba toka waanze kushiriki michuano hiyo na walikabidhiwa kiasi cha shilingi milioni 25 kama zawadi ya mshindi wa kwanza.

error: Content is protected !!