May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yatambulisha mwingine

Spread the love

 

KLABU ya Simba imefanikiwa kunasa saini ya kiungo mshambuliaji wa klabu ya Kagera Sugar, Abdulsamad Kassim mwenye umri wa miaka 24. Anaripoti Mintanga Hunda TUDARCo…(endelea)

Mchezaji huyo ambaye alikuwa moja ya wachezaji nyota ndani ya kikosi cha Kagera Sugar amejiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili.

Abdulsamad ametambulishwa ndani ya klabu hiyo, huku akiwa sehemu ya kikosi hiko kilichopo nchini Morocco kwenye maandalizi (Pre-Season), kuelekea msimu mpya wa mashindano 2021/22.

Simba imeongeza idadi ya kiungo mara baada ya kuondoka kwa Clatous Chama, aliyetimkia nchini Morocco kwenye klabu ya RS Berkane kwa mkataba wa miaka mitatu.

Huu utakuwa usajili wa saba kutambulishwa na klabu ya Simba toka kufunguliwa kwa dirisha kubwa la usajili ambapo litafungwa Agosti 30, mwaka huu.

error: Content is protected !!