May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yashusha kifaa kingine kutoka Senegal

Spread the love

 

KLABU ya Soka ya Simba imefanikiwa kunasa saini ya mchezaji wa kimataifa wa Senegal Pape Ousmane Sakho (24), kuuelekea msimu mpya wa mashindano. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

 Mchezaji huyo ambaye ni winga wa kushoto ametua ndani ya kikosi cha Simba na kujiunga na timu hiyo nchini Morocco ambapo imeweka kambi kujinoa ka msimu ujao.

Simba ipo katika hatua ya mwisho ya kukamilisha usajili wake, kutokana na kufungwa kwa dirisha hilo kimataifa, kabla ya kaunza kutimua vumbi michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika na Ligi ya Mabingwa.

Usajili huo unafanyika katika kuimalisha kikosi hiko ambacho kimeondokewa na wachezaji wake wawili Clatous Chama pamoja na Luis Miquissone.

Chama ambaye tayari amejiunga na klabu ya Barkane ya nchini Morocco kwa mkataba miaka mitatu.

Kwa upande wa Miquissone huwenda muda wowote kutoka sasa akatangazwa kuwa mchezaji mpya wa mabingwa wa Afrika, klabu ya Al Ahly ya nchini Misri.

Sakho amesajiliwa na klabu ya Simba akitokea Teungueth fc, ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu nchini Senegal.

Mchezaji huyo anakwenda kukamilisha idadi ya wachezaji sita waliosajiliwa na Simba mpaka sasa kuelekea msimu ujao huku watatu wakiwa wazawa.

 

error: Content is protected !!