May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yashusha chuma kingine

Spread the love

 

KLABU ya soka ya Simba imefanikiwa kunyaka saini ya kiungo mshambuliaji Jimmyson Mwanuke (18) kutoka klabu ya Gwambina FC yenye maskani yake misungwi, Mwanza. Anaripoti Wiston Josia TUDARCo …(endelea)

Kinda huyo ametambulisha leo Agosti 18, 2021 kupitia kurasa rasmi za klabu hiyo, kwenye mitandao ya kijamii, huku akiwa tayari nchini Morocco kikosi cha timu hiyo kilipoweka kambi.

Mwinuke ambaye alifanya vizuri kwenye msimu uliopita akiwa na klabu ya Gwambina FC, atakuwa anatimiza idadi ya wachezaji wanne wazawa waliosajiliwa na klabu ya Simba mpaka sasa.

Wachezaji wengine wazawa waliosajiliwa na klabu hiyo mpaka sasa ni, Yusuph Muhilu, Abdulsamad Kassim wote kutoka Kagera Sugar na Israel Patrick Mwenda kutoka KMC.

error: Content is protected !!