May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yasajili beki kitasa cha Zimbabwe

Peter Muduhwa

Spread the love

 

KLABU ya Simba imekamilisha usajili wa beki wa kati, Peter Muduhwa raia wa Zimbabwe ambaye alikuwa kwenye michuano ya kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wandani CHAN na timu yake ya taifa inayoendelea nchini Cameroon. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam  …(endelea).

Mchezaji huyo ambaye alikuwa akichezea klabu ya Highlanders FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Zimbabwe, ametambulishwa na klabu ya Simba leo tarehe 26 Januari 2021, ambapo ataitumikia timu hiyo kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa, baada ya usajili wa ndani kufungwa.

Peter Muduhwa

Muduhwa ambaye ametua nchini leo na kusaini mkataba wa miezi sita na mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Usajili wa mchezaji huyo utaifanya Simba mpaka sasa kuwa imesajili wachezaji watatu kwa jili ya michuano hiyo ambayo kwa sasa wamefikia kwenye hatua ya makundi, ambapo mchezo wa kwanza watacheza tarehe 12 Februari 2021 nchini Congo DR dhidi ya AS Vita.

error: Content is protected !!