Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Michezo Simba yarejea mawindoni
Michezo

Simba yarejea mawindoni

Kikosi cha Simba kikifanya mazoezi
Spread the love

 

Maraba baada ya mapumziko siku tano kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara kimeanza tena mazoezi kwa ajili ya ungwe ya mwisho ya michezo ya ligi Kuu Tanzania Bara ambayo inaelekea mwishoni. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Simba iliingia kambini jana huku baadhi ya wachezaji wakiwa kwenye majukumu ya timu zao Taifa ambazo zinataraijia kucheza michezo ya kirafiki hivi karibuni kwa mujibu wa kalenda ya Shiriukisho la mpira wa Miguu Duniani (FIFA)

Wachezaji hao walipewa mapumziko mara baada ya kucheza mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting uliopigwa kwenye Uwanja wa Ccm Kirumba, Mwanza na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Katika mazoezi hayo kikosi cha Simba kitakuwa chini ya kocha wao wa viungo Adel Zrane na kisha baadae kucheza michezo kadhaa ya kirafiki ambayo haikuwekwa wazi kabla ya kurejea kwenye mchezo wa Ligi Kuu tarehe 19 Juni 2021, dhidi ya Polisi Tanzania.

Simba mpaka sasa ndio vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa na pointi 67, mara baada ya kucheza michezo 27 na nafasi ya pili wakiwa watani zao Yanga wakiwa na pointi 61 na michezo 29.

Simba imebakiza michezo mitano kwenye ligi hiyo ambao ni dhidi ya Polisi Tanzania, Azam Fc, Yanga, Mbeya City na Kmc.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Tusua mkwanja na mechi za Ijumaa leo

Spread the love  LEO hii mechi zinaendelea kote na wewe kama unataka...

Michezo

Piga pesa na mechi za EUROPA leo hii

Spread the love Hatimaye Alhamisi ya EUROPA imefika ambapo leo hii mechi...

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

error: Content is protected !!