July 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yaomba kulikimbia ‘shamba la bibi’

Spread the love

BAADA ya kuutumia Uwanja wa Uhuru kwa michezo mitatu ya ligi kuu soka ya Tanzania Bara, uongozi wa klabu ya Simba umeandika barua kwa Shirikisho la soka nchini (TFF) na Wizara ya Habari utamaduni na Michezo ikiomba kuhamishia michezo yake katika Uwanja wa Taifa, anaandika Kelvin Mwaipungu.

Uongozi wa klabu hiyo unaomba kuhamishia michezo yake katika Uwanja wa Taifa badala ya uwanja wa Uhuru kwa madai kuwa ‘vipira’ ambavyo hutumika kama vishikizo vya nyasi bandia katika uwanja huo vimekauku na hivyo kuhatarisha afya za wachezaji wao.

Katika hatua nyingine, uongozi wa klabu hiyo umepokea malalamiko kutoka kwa mashabiki wao, kuhusu msongamano wa watu uliojitokeza katika mchezo wao ligi kuu dhidi ya Azam Fc uliofanyika katika uwanja huo mwishoni wiki iliyoisha.

Hali hiyo imejitokeza kutokana na Mji wa Dar es Salaam kuwa na ongezeko kubwa la watu, hivyo kusababisha kuongezeka kwa idadi ya mashabiki wanaohitaji kuingia uwanjani.

Katika barua hiyo, uongozi wa klabu ya Simba pia umeomba kupata mechi za kujaribu mfumo mpya wa tiketi za kielektroniki, katika siku za Jumatano, Alhamisi na Ijumaa ili mchezo wao wa Jumamosi dhidi ya Majimaji mfumo huo utumike ikiwa ni kabla ya mechi yao na Yanga itakayopigwa Oktoba mosi mwaka huu.

 

error: Content is protected !!