May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba, Yanga zalimwa faini shilingi Mil. 4

Spread the love

 

KAMATI ya uendeshaji na usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu (Kamati ya Saa 72), imezipiga faini klabu za Simba na Yanga jumla ya shilingi milioni nne, katika matukio tofuati yaliyotokea kwenye baadhi ya michezo yao ndani ya Ligi Kuu. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Kwenye kikoa chao walichokaa Aprili 27 mwaka huu, kamati hiyo il;ipitia matukio mbalimbali na mwenendo mzima wa Ligi katika michezo iliyopita hasa mzunguko wa pili.

Vinara wa Ligi klabu ya soka ya Yanga, ilipigwa jumla ya faini ya shilingi milioni 3, kwa maosa mawili tofauti yalijitokeza kwenye mchezo wao namba 151 dhidi ya Azam FC uliopigwa Aprili 6 mwaka huu ambao Yanga waliibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Katika mchezo huo uliofanyika kwenye dimba la Azam complex Chamazi klabu ya soka ya Yanga ilipigwa faini ya shilingi milioni 2, sambamba na onyo kali kwa kosa la kuingia uwanjani na kupitia kwenye mlango usiokuwa rasmi.

Aidha klabu hiyo pia ilitozwa tena faini ya shilingi milioni moja, kwa kosa la mashabiki wake kumrushia chupa mwamuzi msaidizi katika mchezo huo dhidi ya Azam FC na adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 47:1, inayohusu udhibiti wa klabu.

Kwa upande wa klabu ya Simba wao walipigwa faini ya shilingi milioni moja, kwa kosa la mashabiki zao kurusha chupa za maji uwanjani mara baada ya mshambuliaji wao Meddie Kagere kupachika bao kwenye mchjezo dhidi ya Coastal Union.

Mchezo huo ulifanyika Aprili 7 mwaka huu, kwenye dimba la CCM Mkwakwani na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 na adhabu hizo zimetolewa kwa kuzingatia kanuni za 47:1, inayohusu uthibiti wa klabu.

Ndani ya msimu huu si mara ya kwanza kwa klabu za Simba na Yanga, kupigwa faini hizo kutukana na utovu wa nidhamu unaonyeshwa na mashabiki zao haswa wanapokuwa kwenye michrezo ya ugenini.

Aidha katika hatua nyingine kamati hiyo ilizipiga faini klabu za Geita Gold ya shilingi milioni moja kwa kosa la m,ashabiki zao kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, sambamba na kuwaweka kwenye kifungo mashabiki wawili ambao ni Bw. Said Ramadhani na Bw. Omary Kirumbi kutoruhusiwa kuingia uwanjani kwa miezi 12.

error: Content is protected !!