August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba, Yanga wakamia Wajifua usiku na mchana, Nabi, Zoran waumiza vichwa

Spread the love

 

ZIKIWA zimebaki wiki mbili sawa na siku 14, kabla ya klabu za Simba na Yanga kushuka dimbani kwenye mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, klabu hizo zimeonekana kujifua kwa hali na mali katika kutafuta utimamu wa mwili. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Timu hizo zitashiuka dimbani Agosti 13 mwaka huu, kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, katika mchezo wa kuashilia ufunguzi wa msimu mpya wa mshindano.

Mchezo huo utakuwa unawakutanisha miamaba hiyo ya soka nchini katika msimu miwili mfululizo, huku kwenye msimu ulipoita Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0, lilowekwa kambani na Fiston Kalala Mayele.

Kupitia kurasa zao za mitandao mbalimbali ya kijaamii klabu hizo, zimeonesha wachezaji wao wakifanya mazoezi ya utimamu wa mwili kwenye Gym, katika nyakati tofauti.

Simba kwa sasa wao wameweka kambi nchini Misri kwenye mji wa Ismailia, huku mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, klabu ya Yanga wakiamua kusalia jijini Dar es Salaam.

Licha ya klabu hizo mbili kucheza michezo tofauti ya kirafiki kabla ya kukutana, lakini mchezo wa kwanza wa kimashindamno utakauwa baina yao wenyewe kama ilivyokuwa kwenye msimu uliopita.

Kama ilivyoripotiwa na gazeti hili la Raia Mwema, taarifa kutoka nadni ya klabu hizo zimeeleza kuwa makocha wote wawili wapo kwenye presha kubwa kwa sasa katioka kufanya vizuri kwa msimu ujoa.

Katika nyakati tofauti Meneja wa Habari na mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally, wakati wa utambulisho wa kocha huyu wa sasa Zoran Maki, alinukuliwa akisema kuwa malengo ya simba kwa sasa ni kurejesha mataji yote yaliyopotea kwa msimu uliomalizika.

“Malengo ya Simba yapo wazi nay eye ameyakubali, ya kwanza ni kuhakikisha anarejesha mataji yetu mawili tuliyoyapoteza yakiwemo Ligi Kuu na taji la kombe la Shirikisho la Azam, sambamba na ngao ya hisani.” Alinukuliwa Ahmed

Moja ya taji ambalo Simba walikuwa wamelichukua katika kipindi cha miaka miwili, ni taji la Ngao ya hisani ambapo kwa msimu uliopita walilipoteza kwa kukubali kichapo mbele ya Yanga, na hivyo utakuwa mtihani mkubwa kwa kocha Zoran Maki katika kulitetea.

Lakini pia kocha huyo ambaye amepewa kandarasi yam waka mmoja, anatakiwa kluhakikisha timu hiyo inarudi kwenye utawala wake wa kutwaa taji la Ligi Kuu sambamba na kombe la Shirikisho kama ilivyofanya kwenye kipindi cha miaka mine.

Kibarua kikubwa Zaidi kwa Zoran ambacho pengine kinaweza kuhatarisha kazi yake, ni kufanya vizuri kwa klabu hiyo kwenye michuanoa ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa kufika hatua ya nusu fainali.

Kwa upande wa mabingwa watetezi klabu ya Yanga, wao kwa asimilia kubwa wachezaji wao wamesharipoti kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu, ambapo Nabi anakibarua kizito cha kufanya timu hiyo inafanya vizuri tena kwa msimu ujao.

Mara kadhaa aliyekuwa msemaji wa klabu hiyo Haji Manara alijitanabaisha kwa kusema kuwa, Yanga itwaa mataji hayo mara kwa mara katika msimu Zaidi ya sita hivyo mzigo mkubwa katika kutekeleza hilo utabaki kwa Nabi.

“Kwa kikosi hiki tulichokuwa nacho Yanga, tutatwaa mataji haya ya ndani katika msimu sita mpaka 10 mfululizo na hakuna shaka kwenye hilo.” Alisema Manara

Tayari Nabi amesharejea kambini na kuanza maandalizi na kikosi hiko ambacho kimefanya maingizo mapya matano ya wachezaji wakimataifa.

Kama kocha huyo atashindwa kutetea mataji hayo waliyotwaa kwa msimu huu, huwenda nae akawa kwenye wakati mgumu kwa kuwa viongozi wa timu hiyo wakiamia wamempa anachotaka.

error: Content is protected !!