December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba, Yanga kusaka alama tatu nje ya Dar

Cedric Kaze, Kocha wa Yanga

Spread the love

LIGI Kuu Tanzania Bara msimu wa 2020/21 inaendelea tena mwisho wa juma hili ambapo vinara wa ligi hiyo klabu ya Yanga watakuwa ugenini kuwakabili Mwadui FC, huku mabingwa watetezi, Simba wao watakuwa jijini Mbeya kumenyana dhidi ya Mbeya City. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam …  (endelea).

Timu hizo zote zitakuwa nje ya jiji la Dar es Salaam kusaka pointi tatu muhimu ili kujiweka vizuri katika kusaka ubingwa huo.

Tayari kikosi cha Yanga kimeshawasili mkoani Shinyanga toka jana kikitokea Mwanza ambapo waliwasili na ndege kutokea Dar es Salaam huku watani zao Simba wakianza safari mchana huu kuelekea jijini Mbeya.

Yanga wao watashuka dimbani siku ya Jumamosi tarehe 12 Novemba, 2020, kwenye Uwanja wa CCM Kambarage, huku Simba nao watashuka dimbani Jumapili ya terehe 13 Novemba kwenye Uwanja wa Sokoine.

Simba ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi hiyo mara baada ya kucheza michezo 12 wakiwa na pointi 26, nyuma ya Azam FC kwa pointi moja huku wakiwa na michezo miwili mkononi.

Yanga wapo kwenye kilele cha msimamo huo wakiwa na pointi 34 mara baada ya kucheza mechi 14, michezo miwili mbele ya Simba.

Timu hizo mbili zinashuka dimbani huku zikiwa zimefanya vizuri kwenye michezo yao iliyopita ya Ligi Kuu, ambapo Yanga ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Ruvu Shooting, huku Simba akichukua pointi tatu mara baada ya kuwaadhibu Polisi Tanzania kwa mabao 2-0.

Michezo mingine kwenye Ligi hiyo itawakutanisha Mtibwa Sugar dhidi ya KMC, Dodoma jiji itaawalika Gwambina, Polisi Tanzania watajiuliza mbele ya Ruvu Shooting, JKT Tanzania dhidi ya Biashara United, Coastal Union watakuwa nyumbani kuikalibisha Tanzania Prisons.

Ligi hiyo itaendelea tena siku ya Jumatatu ambapo itachezwa michezo miwili ambapo Ihefu FC wataialika Kagera Sugar huku Azam FC watakuwa kwenye dimba la Azam Complex Chamazi kuikalibisha Namungo FC.

error: Content is protected !!