August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba, Yanga kukutana Oktoba 23 Ligi Kuu

Spread the love

 

MECHI inayo vikutanisha vigogo wa soka la Tanzania Simba na Yanga (Kariakoo Derby) katika Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2022/23, inatarajiwa kupigwa Oktoba 23 mwaka huu katika dimba la Benjamini Mkapa majira ya saa 11.00 jioni. Anaripoti Damas Ndelema, TUDARCO … (endelea).

Mechi hiyo ambayo huteka hisia za mashabiki wengi wa soka na kufuatiliwa na watu wengi ndani na nje ya nchi, itakuwa ya nne kukutanisha miamba hiyo ndani ya mwaka mmoja wa 2022. Aprili 30, 2022 walikutana katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na kutoka sare ya bila kufungana, na pia walikutana nusu fainali ya kombe la Shirikisho tarehe 28 Mei, 2022 Yanga ikiibuka na ushindi wa 1-0.

Kabla ya mechi ya tarehe 23 Oktoba, 2022, miamba hiyo itaminyana kwenye mechi ya Ngao ya Hisani tarehe 13 Agosti, 2022.

Mvuto wa mechi hiyo ni kutokana na historia ya timu hizo mbili ikichangiwa na utani wa jadi na tambo za timu hizo kuanzia kwa viongozi mpaka kwa mashabiki wao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano tarehe 3 Agosti, 2022, makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) zilizopo Karume Jijini Dar es Salaam, Ofisa Mtendaji MKuu wa Bodi ya Ligi kuu Almas Kasongo amesema kuwa mechi hiyo baina ya timu hizo itakuwa ni mechi ya raundi ya nane ya msimu wa 2022/23.

Kasongo amesema Ligi kuu ya NBC kuanza rasmi tarehe 15 Agosti mwaka huu na kutamatika tarehe 27 Mei 2023 baada ya mizunguko yote thelathini kuweza kukamilika.
Klabu ya Yanga itafungua msimu kwa kuanzia ugenini katika mchezo dhidi ya Polisi Tanzania huku mahasimu wao Simba wakiwa nyumbani katika Dimba la Benjamin Mkapa dhidi ya Geita Gold ya Geita.

error: Content is protected !!