KUELEKEA mchezo wa fainali wa Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation) siku ya tarehe 25 Julai, 2021, vikosi vya Simba na Yanga vitatumia uwanja mmoja wa mazoezi kwa nyakati tofauti. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Kigoma … (endelea).
Mchezo huo utapigwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika majira ya saa 10 jioni.
Uamuzi huo, umefikiwa mara baada ya kufanyika kwa kikao cha kamati ya mashindano siku ya Jumatatu na kukubaliana timu hizo zitumie Uwanja wa chuo cha Hali ya Hewa, Kigoma.
Yanga ndiyo watakaokuwa wa kwanza kutumia uwanja huo kwenye mazoezi yake ya kwanza toka walipowasili Kigoma, majira ya saa 1 asubuhi kwa usafiri wa Shirika la Ndege la Tanzania.

Simba wao wataanza mazoezi siku ya kesho, baada kutua mkoani Kigoma jioni ya leo wakitokea Dar es Salaam.
Kutumia uwanja huo mmoja kumekuja kufuatia kwa klabu hizo kutoruhusiwa kufanya mazoezi kwenye uwanja wa Lake Tanganyika ambao utachezewa mchezo huo.
Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ndani ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi alisema kuwa hawatoruhusu timu yoyote kutumia uwanja huo mpaka siku ya mchezo.
Leave a comment