August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba, Yanga hapatoshi Mapinduzi Cup

Wachezaji wa Simba na Yanga wakiingia uwanjani katika moja ya pambano lao

Spread the love

HATIMAYE mahasimu wa wawili katika soka la Tanzania, Simba na Yanga wataminyana kesho katika hatua ya nusu fainali kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar baada ya kukamilika kwa michezo ya hatua ya makundi jana.

Simba wanakutana na Yanga baada ya kufanikiwa kumaliza vinara katika kundi A huku nafasi ya pili ikishikwa na timu ya Taifa Jang’ombe ambao walifanikiwa kupata ushindi jana mbele ya mabingwa watetezi URA kutoka nchini Uganda.

Katika mchezo huo utakaopigwa kesho majira ya Saa 2:15 usiku Yanga inaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza kataika mchezo uliomalizika dhidi ya Azam FC baada ya kupata kipigo cha mabao 4-0.

Mchezo wa pili wa nusu fainali utaikutanisha klabu ya Azam FC dhidi ya timu ya Taifa Jang’ombe ambayo ndio timu pekee kutoka visiwani humo kufikia hatua hiyo katika michuano hiyo inayotalajia kukamilika tarehe 12.

error: Content is protected !!