January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba, Yanga hakuna mbabe

Spread the love

 

MTANANGE wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga uliopigwa leo tarehe 11 Disemba 2021, katika dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam, umemalizika kwa sare tasa (0-0). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam  …  (endelea).

Katika mechi hiyo iliyokuwa ya kuvutia, kila timu ilionesha mbinu za hali ya juu kuzuia mashambulizi ya mwenziwe na kuwafanya mashabiki wao kuamini kila moja anaweza kuondoka na ushindi.

Licha ya kipindi cha kwanza Yanga kuonekana kuwa imara haikuambulia kitu licha ya mashuti yake mawili kulenga lango la Simba.

Vivyo hivyo, Simba walionekana kuimarika zaidi kipindi cha pili na kufanya mashambulizi ambapo mashuti matatu yalilenga lango lakini hawakuwa na bahati.

Hadi dakika 90 zinakatika wachezaji watatu wa Simba walikuwa wamelamba kadi za njano huku wawili wa Yanga nao pia wakipewa kadi hizo za onyo.

Umiliki wa mpira unaonesha Yanga wameongeza kwa kuwa na asilimia 51 dhidi ya 49 za Simba.

Hata hivyo, manahodha wa pande zote mbili, Medie Kagere wa Simba na Bakari Mwamnyeto wa Yanga wamekiri kuwa mechi ilikuwa ngumu lakini kwani ilikuwa ni mechi ambayo ilikuwa kiufundi zaidi.

error: Content is protected !!