Tuesday , 23 April 2024
Home Kitengo Michezo Simba, Yanga hakuna mbabe
MichezoTangulizi

Simba, Yanga hakuna mbabe

Spread the love

BAHATI yao! Ndilo neno lililotamalaki katika ndimi za mashabiki wa timu kongwe nchini, Simba na Yanga baada ya leo tarehe 23 Oktoba, 2022 kutoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mbungi hilo lililopigwa muda wa saa 11 jioni katika Uwanja wa Benjamini Mkapa lilikuwa la kukata na shoka huku likichagizwa na mashabiki walioujaza uwanja huo uliopo jijini Dar es Salaam.

Walikuwa wageni wa mcheo huo, Simba ambao waliandika bao la kwanza kupitia kwa kiungo wao mshambuliaji Augustine Okrah raia wa Ghana baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Clatous Chama.

Goli hilo ambalo liwaweka Yanga katika presha kubwa ya mchezo, walisubiri hadi dakika 44 walipojibu mapigo kwa njia ya mpira wa adhabu uliochongwa na Stephane Aziz Ki na kujaa wavuni moja kwa moja.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo kila timu ilitulia na kufanya mashambulizi huku Yanga wakiongoza kwa kulenga lango la wapinzani wao mara sita lakini Simba wakilenga mara mbili.

Simba walipiga nje ya lango mara saba, Yanga mara tano lakini Simba waliongoza kwa kumiliki mpira kwa ujumla kwa asilimia 53.

Katika mechi hiyo iliyosimamiwa na muamuzi wa kati, Ramadhani Kayoko aliyekuwa mkali kwa wachezaji kama pilipili, aligawa kadi kama njugu ambapo wachezaji wanne wa Yanga walipigwa kadi za njano ilihali Simba wakizawadiwa kadi tano.

Hadi dakika 90 zinakatika, timu hizo zilitoshana nguvu, huku Simba ikiendelea kungoza Ligi Kuu bara kwa kufikisha pointi 14 sawa na mtani wake Yanga mwenye pointi 14 lakini wakitofautiana kwa magoli ya kufunga na kufungwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

Michezo

Ujanja ni kubeti na Meridianbet

Spread the love  JUMAPILI ya leo imekaa kihela hela sana ndani ya...

Michezo

Anza Jumamosi yako na mkwanja wa Meridianbet

Spread the loveJumamosi ya leo ODDS zimekaa kijanja sana ndani ya Meridianbet...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

error: Content is protected !!