December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Simba yamtimua Gomes, Hitimana arithi mikoba yake

Didier Gomes da Rosa

Spread the love

 

KLABU ya Soka ya Simba ya jijini Dar es Salaam, imevunja mkataba na aliyekuwa kocha wake Mkuu, Didier Gomes Da Rosa, mara baada ya makubaliano ya pande zote mbili. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Maamuzi hayo yamefikiwa mara baada ya timu hiyo kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana kwenye mchezo uliopigwa jumapili Oktoba 24, 2021 kwenye dimba la Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo imeeleza kuwa, uongozi wa klabu hiyo umeridhia ombi la Gomes juu ya kuachana na Simba kuanzia leo Oktoba 26, 2021.

Mara baada ya kujiweka pembeni nafasi ya Gomes kwenye timu hiyo, itashikiliwa na Thierry Hitimana kama kocha wa muda huku akisaidia na Seleman Matola, kama kocha wake msaidizi.

Aliyekuwa kocha wa makipa wa klabu ya Simba Milton Nienov

Aidha klabu hiyo pia imefanya marekebisho kwenye benchi lake la ufundi kwa kusitiosha mkataba wa aliyekuwa kocha wa makipa Milton Nienov pamoja na kocha wa viungo Aden Zrane.

Gomes alijiunga na Simba January, mwaka huu akitokea kwenye klabu ya El Merreikh ya nchini Sudan, ambapo alikuja kuchukua nafasi ya Sven Vandebroeck aliyetimkia nchini Morocco.

error: Content is protected !!