January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yamtangaza mrithi wa Nienov

Spread the love

 

LEO Disemba 7, 2021 klabu ya soka ya Simba imemtangaza Tyron Damons Raia wa Afrika kusini kuwa kocha mpya wa makipa, akija kuchukua mikoba ya Milton Nienovambaye mkataba wake ulivunjwa na uongozi wa klabu hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Simba imemtangaza kocha huyo siku chache mara baada ya kufuzu kwa hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho Barani Afrika kwa kuwaondosha Red Arrows ya nchini Zambia.

Kocha huyo mpya wa makipa amejiunga na Simba akitokea nchini Afrika Kusini kwenye klabu ya Chippa United ya nchini Afrika Kusini.

Tyron analeseni ya daraja D na C, kutoka kwenye Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’

Mara baada ya kujiunga na Simba, hii itakuwa klabu yake ya nne kuwa kocha namba moja wa makipa toka mwaka 2013, alipoanza kazi hiyo rasmi.

Klabu ya kwanza kupita kocha huyo ilkuwa Bidvest Wist ya nchini Afrika Kusini kuanzia mwaka 2013 mpaka mwaka 2020, na kisha kutimkia kwenye klabu ya TS Galaxy ambapo alidumu kwa mwaka mmoja tu mpaka 2021, kisha alijiunga na Chippa United.

Kocha huyo anakwenda kuwanao makipa wanne kwenye klabu hiyo ambao ni Aishi Manula, Beno Kakolanya, Jeremiah Kisubi na Ally Salim.

error: Content is protected !!