May 21, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yamtambulisha Mfaransa kuwa kocha mpya

Didier Gomez, Kocha Mpya wa Simba (kushoto) akiwa na Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Barbara Gonzalez wakionyesha mkataba waliosaini kukinoa kikosi hicho

Spread the love

 

UONGOZI wa klabu Simba umemtambulisha, Didier Gomes raia wa Ufaransa kuwa kocha mpya wa klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Kocha huyo ambaye alifika jana nchini akitokea Sudan ambapo alikuwa akifundisha klabu ya Al Mereikh ambayo ipo na Simba kwenye kundi moja kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari jijini Dar es salaam wakati wa kumtambulisha kocha huyo, Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba, Barbara Gonzalez amesema walipokea jumla ya wasifu wa makocha 70, lakini baada ya kuwachambua walifikia maamuzi ya kumuajiri Gomes.

“Tulipata maombi zaidi ya 70 na tukafanya usahili kupitia kwenye bodi na watu wa benchi la ufundi na baadaye tukafanya maamuzi,” amesema Barbara.

Mara baada ya kusaini mkataba kocha huyo, amesema anafuraha kujiunga na Simba kutokana na kuwa moja ya timu yenye mashabiki wengi nchini pamoja na malengo makubwa.

“Ninafuraha kuwa na nyie leo kwa sababu Simba ni timu yenye mashabiki wengi na inatarajia kufanya makubwa sana kwa mwaka huu,” amesema Gomez, kocha mpya Simba.

Mara baada ya kujiunga na timu hiyo Gomes ataanza kazi hii leo kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya kombe la Simba itakayoanza 26 Januari 2021, ambayo itashirikisha timu tatu.

error: Content is protected !!