Thursday , 18 April 2024
Home Kitengo Michezo Simba yamshitaki Mzee Kilomoni TFF
Michezo

Simba yamshitaki Mzee Kilomoni TFF

Mzee Hamisi Kilomoni
Spread the love

KLABU ya Simba imemfikisha Mzee Hamisi Kilomoni, aliyekuwa Mjumbe wa Bodi yake ya  Wadhamini katika Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ikimtuhumu kukiuka sheria. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 16 Julai 2019 jijini Dar es Salaam, Crescentius Magori, Afisa Mtendaji Mkuu Simba amedai kuwa, Mzee Kilomoni anakiuka sheria za nchi na TFF kwa kuudanganya umma ya kwamba yeye ni mdhamini wa Simba wakati alishavuliwa wadhifa huo.

“Hapa karibuni tumekuwa na taarifa mbalimbali sana kuhusu aliyekuwa mdhamini wetu wa Simba, Mzee Kilomoni, amezunguka kwenye vyombo vya habari akisema ni mdhamini, alikotupeleka tulikuwa hatutaki kwenda.

“Sababu Simba ni taasisi, tunaona lazima tuzungumze na leo nimekuja na barua kuonyesha kwamba Mzee Kilomoni si mdhamini wa Simba, sababu kuna watu hadi leo hawaamini wanaamini Kilomoni anasema ukweli,” amesema Magori.

Magori amesema Mzee Kilomoni alivuliwa udhamini wa bodi ya wadhamini ya Simba tangu mwezi Oktoba mwaka 2017 na kupewa taarifa rasmi kupitia barua tarehe 8 Novemba mwaka huo.

“Pimeni hili, huyu mzee sio mdhamini wa Simba anatumia nafasi kudanganya watu na vyombo vya habari, na sisi sababu tunajua anafanya maamuzi, tuliwapeleka barua katika kamati ya maadili ya TFF itamuita, itamhoji atajieleza, sababu sisi hatupendi malumbano,” amesema Magori na kuongeza.

“Lakini Mzee Kilomoni hafuati taratibu na sheria za nchi, mwanasheria wale alithibitishiwa kuwa sio mdhamini lakini anaendelea kudanganya watu, akiongea yeye kama mtu mwingine aongee lakini akiongea kama mdhamini hilo tulishafunga.”

Kuhusu sakata la Mzee Kilomoni kung’ang’ania hati za mali za Simba, Magori amesema uongozi wa klabu hiyo unafanya mchakato wa kitangaza katika magazeti ya serikali kwamba zimepotea ili wapatiwe nyingine.

“Alikuwa na hati moja ya majengo ya Simba, lakini yana hati 2, wadhamini wenzake wameenda kumuomba mara aseme atakupa mara wanangu waje watafute, sisi tutangaza kwenye magazeti ya serikali imepotea.

“Kwa nini ung’ang’anie, ameshikilia kwa makusudi atadhani anatukwamisha, mtu aliyekuwa anamshauri ang’ang’anie hakumshauri vyema,” amesema Magori.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

Michezo

TFF, Amrouche ngoma nzito

Spread the loveVIPENGELE vya mkataba wa kazi aliotia saini Kocha Mkuu wa...

error: Content is protected !!