Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Michezo Simba yampiga ‘Stop’ Mkude
Michezo

Simba yampiga ‘Stop’ Mkude

Jonas Mkude
Spread the love

UONGOZI wa klabu ya Simba umemsimamisha kiungo wake mkabaji, Jonas Mkude kwa muda wa siku zisizojulikana kutokana na utovu wa nidhamu mpaka atakaposilizwa kwenye kamati ya nidhamu ya klabu hiyo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezaji huyo ni moja ya wachezaji waandamizi kwenye kikosi hiko kwa sasa ambaye amehudumu kwa miaka nane, amesimamishwa bila kuanishwa aina ya makosa aliyoyafanya kiasi cha kupelekea uongozi huo kumchukulia hatua.

Taarifa iliyotolewa kutoka ndani ya klabu hiyo na mtendaji wake mkuu, Barbara Gonzalez imeeleza kuwa mchezaji huyo atapalekwa kwenye kamati ya nidhamu ya klabu ili kila pande ipate haki ya kusilizwa kabla ya kutoa uamuzi.

Hii itakuwa mara ya pili kwa mchezaji huyo kufikishwa kwenye kamati ya nidhamu ya klabu hiyo, ikumbukwe mara ya kwanza ilikuwa tarehe 9 Oktoba, 2019 mara baada ya Mkude na wenzake kutakiwa kufika mbele ya kamati hiyo iliwaweze kujieleza.

Wachezaji wengine waliofika mbele ya kamati hiyo alikuwa ni Gadiel Michael, Erasto Nyoni na Clotous Chama kwa kosa la kuchelewa kambini na kukosa michezo miwili ya Ligi kuu kanda ya Ziwa dhidi ya Kagera Sugar na Biashara United kwenye msimu wa 2019/20.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!