Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Michezo Simba yamkana Manara, kuchukua hatua
Michezo

Simba yamkana Manara, kuchukua hatua

Haji Manara
Spread the love

KLABU ya soka ya Simba imemkana Afisa habari wake, Haji Manara kufuatia kauli yake yakutotaka mashabiki wa timu pinzani kuja kwenye mchezo dhidi ya Plateau huku uongozi wa klabu hiyo ukisema kuwa kauli hiyo sio msimamo wa Taasisi kama ilivyoelezwa hapo awali na watachukua hatua. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Akiongea mbele ya waandishi wa habari kwenye mkutano ulioitishwa na klabu ya Simba huku akiwa ameongozana na Kaimu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Mwina Kaduguda kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Manara alinukuliwa akisema kuwa hawatoruhusu shabiki asiyekuwa wa Simba kuja kuwazomea au kuwaletea tabu kwenye mchezo huo.

“Hatutoruhusu jezi isiyokuwa nyeupe na nyekundu uwanjani, kama unataka kutuzomea kaa pembeni nah ii ni kauli ya Simba hatuwezi kuruhusu mtu atuletee tabu,” alisema Manara.

Mchezo huo wa raundi ya pili ya michuano ya kombe la klabu bingwa barani Afrika kwenye hatua ya awali utachezwa siku ya Jumamosi kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam majira ya saa 11 kamili jioni.

Kufuatia kauli hiyo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikemea swala hilo na kutoa kauli ya kuwa, kwa mujibu wa katiba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Dunia (Fifa) na TFF imeeleza kuwa vitendo vya ubaguzi wa aina yoyote havitakiwi kwenye mpira wa miguu.

Taarifa kutoka TFF iliendelea kwa kueleza kuwa shabiki yoyote anaruhusiwa kuingia kwenye mchezo wa mpira wa miguu nchini ikiwa tu havunji sheria na taratibu za mchezo huo.

Kikao cha Bodi ya Simba

Kufuatia kulaani huko kwa TFF, uongozi wa klabu ya Simba ukatoa taarifa kwa umma na kueleza kuwa kauli hiyo iliyotolewa na msemaji wao iliyoashilia kuzuia baadhi ya mashabiki kufika uwanjani kuangalia mchezo huo haikutolewa kwa maelekezo ya klabu na kuhakikisha kuwa suala hilo halitokei tena.

Aidha Taarifa hiyo iliendelea kueleza kuwa klabu hiyo inawakaribisha mashabiki wote na hata ambao watakuja kuwashangilia wageni kwenye mchezo huo imewahakikishia kwamba haitawazuia na wala kupata bugudha yoyote.

Simba inaingia kwenye mchezo huo huku ikiwa na faida ya ushindi wa bao 1-0, kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa mjini Jos, Nigeria kwa bao lilifungwa na Clatous Chama dakika ya 53.’

Plateau United wanatarajia kuingia nchini siku ya kesho kwa ajili ya mchezo huo ambao Simba wanahitaji sare au ushindi wa aina yoyote kuweza kusonga mbele kwenye hatua ya mzunguko wa kwanza ambapo atakutana na Platnumz ya Zimbabwe au Costa do Sol kutoka Msumbiji.

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & UchambuziMichezo

TFF kuamua hatima ya Amrouche

Spread the loveHATIMA ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche kuendelea...

Habari za SiasaMichezo

Matinyi: Dk. Ndumbaro alifanya utani ukaguzi mechi za Yanga, Simba

Spread the loveMsemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema kauli iliyotolewa na...

Michezo

Gethsemane Group Kinondoni (GGK) waachia video ya Bwana Wastahili

Spread the loveWAIMBAJI maarufu nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video...

BiasharaMichezo

Gamondi kocha bora mwezi Februari, NBC yamjaza manoti

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!