May 21, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yambakisha Tshabalala

Spread the love

Baada ya tetesi nyingi hatimaye klabu ya Simba imemuongezea mkataba beki wake wa kushoto Mohammed Hussen ‘Tshabalala’. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa kutoka kwenye ukurasa wao kwenye mtandao wa Kijamii wa Instagram wameweka picha ya mchezaji huyo akisaini mkataba mpya na kuandika kuwa “Bado yupo Sana.”

 

Hivi karibuni kulikuwa na taarifa za kuwa huwenda mchezaji huyo akatimkia upande wa pili wa mapinzani wao klabu ya Yanga mara baada ya mchezaji huyo mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Katika taarifa yao hiyo Simba haikueleza mchezaji huyo ameongeza mkataba katika kipindi cha muda gani wala kutaja thamani ya mkataba huo.

error: Content is protected !!