May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yambakisha Kapombe

Spread the love

 

MABIGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba ya jijini Dar es Salaam, imemwongezea mkataba beki wake kisiki, Shomari Kapombe. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam …(endelea). 

Ni mwendelezo wa vinara hao wa ligi kuu, kuwaongezea mikataba wachezaji wake iliyokuwa inakwenda kumalizika mwishoni mwa msimu huu wa 2020/21.

Leo asubuhi Ijumaa, tarehe 30 Aprili 2021, mitandao ya wanarobo fainali hao wa Klabu Bingwa Afrika, wameweka picha za Kapombe akisaini huku kando akiwa na Kocha Msaidizi, Suleiman Matola.

Picha hizo, zimeambatana na maneno “beki bora wa kulia nchini, Shomari Kapombe amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuichezea Simba SC.”

Wengine walioogezewa mkataba ndani ya wiki hii ni; beki wa kushoto, Mohamed Hussein maarufu Tshabalala na Nahodha wa timu hiyo, John Bocco.

error: Content is protected !!