
VINARA wa Kundi A wa michuano ya Klabu Bingwa Afria, Simba ya Tanzania, imetoka sare ya bila kufungana na Al Merrikh, katika Uwanja wa Omdurman, nchini Sudan. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)
Mchezo huo umechezwa leo Jumamosi tarehe 6 Machi 2021, na kuwafanya Simba, kufikisha pointi saba katika kundi hilo, kati ya michezo mitatu iliyokwisha kucheza.
Nafasi ya pili inashikwa na As Vital ya Congo ikiwa na pointi tatu sawa na Al Ahly ya Mirsi huku Al Merrikh ikiwa mkiani kwa pointi moja.
Michezo miwili ya awali ya Simba ilikwenda Congo kucheza na As Vital na kuibuka ushindi wa 1-0 na mchezo uliofuata ilicheza nyumbani, Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam, dhidi ya Al Ahly na kuibuka na ushindi wa 1-0.
Saa 4:00 usiku leo Jumamosi, Al Ahly watakuwa nyumbani kucheza na As Vital kwenye mchezo mwingine wa kundi hilo.
More Stories
Mayele atetema Mwanza, mabao 14 sawa na Mpole
Kim aita 28 Stars
Mauya miwili tena Yanga