January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yakata ngebe za Yanga, Okwi kidume

Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi

Spread the love

SIMBA leo imeendeleza ubabe kwa watani wao, Yanga SC baada ya kuwafunga bao 1-0 katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, huku mshambuliaji wake, Emmanuel Okwi akiibuka shujaa. Anaripoti Erasto Stanslaus … (endelea).

Shukrani kwa Okwi aliyefunga bao hilo pekee kipindi cha pili. Mshambuliaji huyo alikuwa hajaifunga Yanga tangu arudi katika timu yake akitokea katika klabu hiyo ya Jangwani.

Mchezo huo uliochezeshwa na Martin Saanya wa Morogoro, alimtoa nje kwa kadi nyekundu kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima baada ya kuoneshwa kadi ya pili ya njano.

Okwi alifunga bao pekee katika mchezo huo dakika ya 52 kwa shuti la umbali wa zaidi ya 22 akimalizia pasi ya Said Ndemla, na mpira huo kumshinda kipa Ally Mustafa ‘Barthez’

Ushindi huo umechochea mbio za ubingwa kwa Simba SC kwani sasa imefikisha pointi 26 baada ya kucheza mechi 17 na kupanda hadi nafasi ya tatu nyuma ya Azam FC yenye pointi 30 na Yanga 31.

Simba sasa imerejea rasmi katika mbio za ubingwa, kwani iwapo itaendelea kufanya vizuri na wapinzani Azam na Yanga wakateleza, mambo yanaweza kugeuka.

error: Content is protected !!