May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yajitolea kutangaza Utalii Tanzania

Spread the love

 

UONGOZI wa klabu ya Simba umekubaliana na Wizara ya Maliasili na Utalii kutangaza nchi kupitia jezi zao watakazotumia kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Simba kwa sasa ipo kwenye hatua ya makundi kwenye michuano hiyo ambapo itaanza kampeni yake dhidi ya AS Vita mchezo utakaochezwa tarehe 12 Februari 2021, nchini DR Congo.

Klabu ya Simba pamoja na Wizara ya Maliasili na utalii waimengia makubaliano leo tarehe 5 Februari 2021, jijini Dodoma ambapo mbele ya jezi ya samba kutakuwa na maneno yalioandikwa ‘Visit Tanznaia (yenye maana Tembelea Tanzania) ikiwa na lengo la kukuza sekta ya utalii nchini.

Akiongea wakati wa kusaini makubaliano hayo Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa wao kama klabu wanawajibu wa kuitangaza nchi kupitia michuano hii mikubwa barani Afrika.

“Sisi ni wajibu wetu kama Watanzania kutangaza nchi yetu, tumeona tuna nafasi kwenye Ligi ya Mabingwa  kwa kuingia hatua ya makundi na Simba imeona umuhimu wa kutangaza nchi yetu kupitia michuano hiyo ambayo inatazamwa na watu wengi,” alisema Barbara.

Kwa upande wa Wizara kupitia kwa Waziri, Dk. Damas Ndumbaro wameleeza kuwa wanaishukuru klabu ya Simba kwa kujitolea kwao kutangaza utalii wa nchi kupitia michuano hiyo ambayo inafuatiliwa na watu wengi.

“Tunapenda kuipongeza Simba kwa sababu wameingia kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo inatazamwa na watu wengi na wamekuja wenyewe kuomba kitangaza nchi na sisi kama serikali tumepokea ofa hiyo na kukubali kuweka neon ‘Visit Tanzania’ mbele ya jezi zao,” alisema waziri huyo.

error: Content is protected !!