Wednesday , 29 March 2023
Home Kitengo Michezo Simba yajibu mapigo FCC, yatoa ufafanuzi wa Bil. 20
Michezo

Simba yajibu mapigo FCC, yatoa ufafanuzi wa Bil. 20

Kikao cha Bodi ya Simba
Spread the love

KLABU ya soka ya Simba imetolea ufafanuzi taarifa iliyotolewa na Tume ya Ushindani ya Kibiashara (FCC) na kueleza mwekezaji wao, Mohammed Dewji (MO) alisema kuwa mchakato wa mabadiliko wa klabu hiyo upo mikononi mwa FCC na siyo tume hiyo imekwamisha au kuchelewesha mchakato huo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Jana 19 Novemba 2020, FCC ilitoa taarifa kwa Umma ikieleza kuwa mchakato mabadiliko wa klabu hiyo kwenda kwenye mfumo wa hisa umekwamishwa na Simba wenyewe kwa kushindwa kuwasilisha nyaraka walizoombwa na tume hiyo kwa ajili ya kukamilisha uchunguzi.

Kwenye Taarifa ambayo klabu ya Simba wameitoa hii leo tarehe 20 Novemba, 2020, imeeleza mambo mengi ikiwamo toka kuanza kwa mchakato huo, huku wakitolea ufafanuzi kiasi cha pesa kinachopaswa kuwekwa ambacho kimeainishwa kwenye mkataba wa makubaliano (memorandum of understanding) ambao uliwasilishwa FCC ambacho mwekezaji anapaswa kutoa.

FCC walitaka maelezo ya kwanini kiasi kilichotajwa kwenye mkataba wa makubaliano ambacho mwekezaji anapaswa atoe ni tofauti na wanachosikia kwenye vyombo mbalimbali vya Habari.

Klabu ya Simba imeeleza kuwa kamati huru iliyoundwa ilikuwa ikitathimini thamani ya zabauni na kuanisha kuwa thamani ya asilimia 50 ya kampuni iliyoundwa kwa pamoja kati ya mwekezaji na klabu ni Sh. 20 bilioni na mwekezaji pekee aliyeshinda zabuni hiyo ni Mohamed Dewji.

Mohamed Dewji (MO)

Aidha taarifa hiyo iliendelea kwa kueleza kuwa mara baada ya serikali kutoa maelekezo mapya ya kuwa mwekezajia apewe asilimia 49, makubaliano ya mkataba wa makubaliano kati ya klabu na mwekezaji yalikuwa mwekezaji atatoa Sh. 19.6 bilioni baada ya mchakato kukamilika.

Licha ya kutolea ufafanuzi kiasi halisi cha fedha kinachopaswa kuwekwa, Simba pia ilitolea ufafanuzi wa barua mbalimbali walizoandikiwa na FCC sambamba na vikao mbalimbali walivyofanya kufanikisha mchakato huo.

Pamoja na sintofahamu hiyo lakini Simba wameeleza wataendelea kutoa ushirikiano na tume hiyo kwa kuwa wanaamini jambo hili ni jipya kwa klabu kwenda kwenye mfumo wa uwekezaji hivyo litakuwa na changamoto nyingi lakini wanaamini litafikia mwisho mzuri.

Simba ndio klabu ya kwanza nchii hii kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa klabu kutoka kwa wanachama kwenda kwenye kampuni kwa kuuza hisa, jambo litakalofanikisha Simba kujiendesha kisasa na kibiashara.

Tarehe 3 Decemba, 2017 mfanyabiashara Mohamed Dewji alishinda zabuni ndani ya klabu hiyo kwa kupata hisa asilimia 49, kwa kiasi cha Sh. 20 bilioni, katika mchakato uliondeshwa na kamati maalumu ya mabadiliko ya klabu hiyo iliyokuwa chini ya Jaji Mihayo.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

TANROADS wawataka watumishi wazingatie michezo kazini

Spread the love  WAKALA wa barabara Tanzania (TANROADS) imesema michezo inapaswa kuzingatiwa...

Michezo

Yanga: Fedha za Rais Samia zinaleta ari kubwa

Spread the loveUONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema fedha zinazotolewa na Rais...

Michezo

Simba Sc. yamvulia kofia Rais Samia, yamuahidi makubwa dhidi ya Horoya

Spread the loveWAKATI timu ya Simba ikiibuka na ushindi wa bao 3-0...

Michezo

Taasisi ya TKO na TFF yawapiga msasa makocha wa kike 54

Spread the love WAKATI Soka la wasichana likichipua kwa kasi Taasisi ya...

error: Content is protected !!