July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yaitumia salamu Yanga, yainyuka Prisons 5-0

Mfungaji wa mabao matatu, Ibrahim Hajibu akiwapungia mashabiki wa Simba, kulia ni Ramadhan Singano na Danny Sserunkuma

Spread the love

SALAMU ziwafikie. Ushindi mnono wa mabao 5-0 walioupata timu ya Simba dhidi ya Prisons ni salamu kwa watani wao Yanga kuelekea katika mchezo wao utakaochezwa Machi 8, 2015 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Anaripoti Erasto Stanslaus … (endelea).

Simba ambao wamezinduka katika mchezo huo uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa baada ya kutoka kwenye kipigo cha 1-0 cha Stand United, watakutana na Yanga mwishoni mwa wiki ijayo katika mechi ya mzunguko wa pili wa ligi hiyo.

Kwa ushindi huo Simba sasa inatimiza pointi 23, baada ya mechi 16, ingawa inabaki nafasi ya nne nyuma ya Kagera Sugar yenye pointi 24, Azam FC pointi 27 na Yanga 31.

Shukrani kwa mabao matatu yaliyofungwa na Ibrahim Hajibu, alifunga bao la kwanza dakika ya 15 akimalizia pasi nzuri ya Mganda, Dan Sserunkuma, akafunga la pili dakika ya 21 akimalizia mpira uliotemwa na kipa wa Priosns, Mohammed Yussuf, kufuatia shuti la Emmanuel Okwi.

Hajibu alikamilisha hat-trick yake dakika ya 41 kwa mkwaju wa penalti, baada ya beki wa Prisons, Lugano Mwangama.

Mabao mengine ya Simba yamefungwa na Okwi dakika ya ya 75 kwa shuti kali akimalizia kazi nzuri ya Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na Ramadhani Singano ‘Messi’ akapigilia msumari wa mwisho dakika ya 84 akimalizia krosi ya Okwi.

error: Content is protected !!