June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yaipumulia Azam, yaipiga 2-1 Kagera

Kiungo wa Simba, Ramadhani Singano 'Messi' (kulia) akishangilia moja ya bao lake akiwa na Hassan Isihaka

Spread the love

TIMU ya Simba leo imepunguza wigo wa pointi kati ya wapinzani wake wa mbio za Ubingwa msimu huu, Azam na Yanga baada ya kuitandika Kagera Sugar mabao 2-1 katika mchezo wa kiporo uliochezwa kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. Anaripoti Erasto Stanslaus … (endelea).

Mchezo huo awali ulipangwa kuchezwa Jumamosi iliyopita lakini ilishindikana kutokana na uwanja huo kujaa maji hivyo, ukachezwa leo jioni na kumalizika kwa matokeo hayo.

Kutokana na ushindi huo Simba imebaki katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 35 ikiwa ni tofauti ya pointi moja ya Azam FC iliyokuwa nafasi ya pili, Yanga inaoongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 40, tofauti ya pointi tano na Simba.

Mabao ya Simba katika mchezo huo wa 21, yamefungwa na Ramadhani Singano na Ibrahim Hajib kwa mkwaju wa penalti wakati bao la Kagera limefungwa na Rashidi Mandawa.

Katika mchezo mwingineulioshindwa kumalizika jana kwenye uwanja huo kutokana na mvua, kati ya Stand United na Mtibwa Sugar umemaliziwa leo asubuhi, huku matokeo yakibaki 1-0 kama yalivyokuwa jana, bao hilo lilifungwa na Haruna Chanongo.

error: Content is protected !!