December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Simba yaipiga Ruvu 3-1, aliyeitoboa Yanga, aitoboa Simba

Spread the love

 

MABINGWA watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara, Simba ya jijini Dar es Salaam, imejipatia ushindi mnono wa 3-1 dhidi ya Ruvu Shooting. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo umechezwa leo Ijumaa, tarehe 19 Novemba 2021 katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Simba ikicheza kandanda safi kipindi cha kwanza chini ya kocha wake mpya, Pablp Martin imejipatia goli kwa kwanza dakika ya 17 kupitia kwa Meddie Kagere.

Huku ikiendelea kulisakama lango la Ruvu Shooting, Kagere tena aliingia wavuni dakika ya 36 na kumfanya kufikisha magoli manne na kuongoza kwa ufungaji wa magoli katika ligi hiyo.

Ikiwa bado na uchu wa magoli, mshambuliaji wake Kibu Denis aliiandikia Simba bao la tatu dakika ya 44 na kuwafanya kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa magoli 3-0.

Kipindi cha kwanza kilipoanza, timu zote zilishambuliana kwa zamu huku Ruvu Shooting wakionekana kulisakama zaidi lango la Simba.

Dakika ya 70, yule yule aliyekata mzizi wa kutofungwa kwa Yanga, Shaban Msala amefanya hivyo kwa Simba kwa kuwafunga bao maridadi lililomshinda kipa wa Simba, Aishi Manula.

Yanga ilikuwa imecheza michezo minne pasina lango lake kuruhusu bao hadi Masala alipokuja kuwafunga.

Aidha, imeshuhudia Erasto Nyoni wa Simba akikosa penati baada ya mkwaju huo kupanguliwa na Mohamed Makaka.

Ushindi huo kwa Simba imewafanya kufikisha pointi 14 kati ya michezo sita iliyocheza huku watani zao Yanga ikisalia kileleni kwa pointi 15 kati ya michezo mitano iliyocheza na kesho Yanga itacheza na Namungo, mkoani Lindi.

error: Content is protected !!